(HATARI! KUWA MAKINI) HIVI NDIVYO MAWAZO YAKO YANAVYOUMBA.

KANUNI YA UVUTANO
Siri hii imefichwa kwa miaka mingi na watu wachache, labda kwa tamaa ya kutawala wengine, Lakini sasa leo hii naiweka wazi mbele yako.! Itumie.

Muumbaji alipoumba ulimwengu aliweka kanuni za asili pia kanuni za maumbile. Mfano ukirusha jiwe juu ni lazima lirudi kwasababu ya kanuni ya kani ya uvutano ya dunia. 
Kanuni hiyo haifikiri fikiri bali inatenda kazi papo hapo!

Sasa Siri kubwa ni kwamba ipo pia kanuni ya uvutano isiyoonekana kwa macho inayoitikia mawazo yako yote na hata maneno na matendo yako yote. 
Kanuni hii ni kama kani ya uvutano kidunia kiutendaji kwani haifikiri wala kusubiri bali inatenda kama ilivyoumbwa. kila unachowaza kichwani mwako iwe kwa kujua au kutojua unakua umeichokoza kanuni hii na yenyewe huanza kazi mara moja.

Ukiwaza afya au pesa utaipata, ukiwaza ajali itakupata, ukiwaza umaskini utaupata, ukiwaza kufaulu, matatizo, ugomvi, amani n.k kwahiyo maisha yetu kwa asilimia kubwa ni vile tunavyojiwazia. Tumepewa uwezo wa kuumba.

Kanuni hii pia haiyaachi matendo yetu hivihivi, kila tendo unalotenda kanuni hii ya uvutano inakuletea mambo yanayofanana na matendo yako, mfano ukitenda wema utakurudia, na hata ukitenda ubaya kanuni hii haiangalii wewe ni nani na wala haiangalii usoni ubaya huo utakurudia tu.! hata iwaje.

kingine ni kwamba ukiwa na tabia ya kushukuru kanuni hii inaleta mambo ya kushukuru zaidi.
Ukiwa na tabia ya lawama kanuni hii itaendelea kukuletea zaidi na zaidi mambo yale yatakayokufanya ulalamike.

Asilimia kubwa ya watu duniani kote wanaishi maisha ya maumivu sababu ya kutojua chochote kuhusu kanuni hii ya asili. mfano mtu anaweza kukiri kwa mdomo wake kua yeye ni mzembe. kanuni hii huwa haifanyi mzaha bali huleta hali hiyo kweli. 
Ndugu msomaji unapokiri lolote kwa kutamka au kwa kuwaza jua kua unaumba.
Kwa maana hiyo watu wengi wanateseka na magonjwa, matatizo na majanga ambayo wamejiumbia wenyewe.

Kanuni hii haijali kama wewe unatambua uwepo wake au hutambui, yenyewe inafanya kazi vile ilivyoumbwa. kuijua kwako au kutoijua hakuathiri utendaji wake.

#KanuniYaUvutano
#NguvuYaAkili
#Kujitambua
#SelfRealization 
#AmkaUangaze

(BOFYA HAPA KUSOMA baadhi yaMiujiza iletwayo na tabia ya kushukuru)



Share on Google Plus

About Unknown

NyangeTech inahamasisha maelfu na maelfu ya watu kujitambua kuelekea safari ya kuangaziwa ili kupata utulivu wa nafsi kwa kupata muunganiko na Mungu.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment