(SIRI) Akunyang'anyaye Simu Mpe na Powerbank Pia !



Mara ya mwisho kuamini ilikua lini?
Je unayaamini maisha? Je unawaamini watu na vitu vyoye?. Hii ni Siri, Mungu yupo kila sehemu, hata ndani ya watu na vitu vyote yumo!.
Unapoviamini vitu au unapowaamini watu bila kujali tabia zao kwamba ni waaminifu au sio waaminifu, moja kwa moja unaingia kwenye chaneli ya kuwa mmoja wa wamwaminio Mungu.

Amini kila mtu na kila jambo kisha jifunze kuachilia.  Je Umeumizwa na mtu au watu? basi Usipoteze imani, kuamini hata kuumizwa huko kwani hakuna jambo lisilo na sababu, amini kuna kitu asili imekusudia kwako. Hivyo Achana nao waliokuumiza na wasamehe kabisa, ishi maisha yako.
 Je umeibiwa simu? muamini mwizi  mfuate kwa upendo mpe chaja na powerbank yako pia, Kwasababu kuna wakati Mungu anataka kusema nawe ila masikio yako ya kiroho yamezibwa na vitu unavyovimiliki (mali).


#letGo
#Kutoshikamana
#Surrender 
#TrustTheUniverse
#SelfRealization
#Spirituality
#AmkaUangaze

Share on Google Plus

About Unknown

NyangeTech inahamasisha maelfu na maelfu ya watu kujitambua kuelekea safari ya kuangaziwa ili kupata utulivu wa nafsi kwa kupata muunganiko na Mungu.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment