(SIRI) FANYA HIVI KISHA MAPUNGUFU YOTE ULIYONAYO YATAPOTEA YENYEWE.

Jipende asilimia mia moja (100%) haijalishi watu wanasemaje kuhusu wewe. Haijalishi dini zinasemaje kuhusu wewe. Haijalishi unajiona una mapungufu kiasi gani, jipende hivyohivyo 100% hayo yote yatamezwa automatic utakapoanza kuitumia SIRI hii ya kujipenda.

Tunaishi kwenye wakati wa vichaa, karibu kila mtu ameacha kujipenda halafu anatafuta mtu wa kumpenda kuziba pengo. Anayempata nae hajipendi hivyo lengo halitimii, (Atakumulikiaje wewe wakati hata yeye hana mwanga?) hivyo zinazalika vita, lawama, msongo wa mawazo (stress), majuto, uadui, na magonjwa kama vidonda vya tumbo, magonjwa ya moyo na akili.

Siri nyingine ni kwamba ukifanikiwa kujipenda kumpenda jirani yako huwa kunakuja automatic hata kama hutaki. (Lisipotokea hili jua umekosea njia na unaidanganya nafsi yako hivyo anza upya kujipenda kwa upendo sahihi mpaka ufanikiwe). 
Nkutakie kila la kheri.

#Jipende
#Jikubali
#SelfAcceptance
#AmkaUangaze
# SelfLove
#Spirituality
#Kujitambua 
#SelfTransformation
Share on Google Plus

About Unknown

NyangeTech inahamasisha maelfu na maelfu ya watu kujitambua kuelekea safari ya kuangaziwa ili kupata utulivu wa nafsi kwa kupata muunganiko na Mungu.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment