(SIRI) Wewe sio huo mwili, huo mwili ni wako!

Je ushawahi kujiuliza wewe ni nani?, ngoja nikupe siri, Karibu vyote unavyofikiria hivyo sio wewe! wewe sio cheo chako, wewe sio kazi yako, wewe sio huo mwili, huo mwili ni wako unaumiliki hivyo basi kamwe huwezi kua unachokimiliki.
Nionavyo mimi hakuna dhambi yoyote nyingine ila kushikamana na mwili.
Ndio hii nakuibia siri nzito, kuiba, kuua, uongo, chuki, kuabudu vitu vya ajabu, kutokua na maadili n.k Zote hizo sio dhambi, dhambi ni moja tu Kushikamana na mwili (Attachment) Hii ndiyo inataga hayo yote hapo juu ambayo kwa karne nyingi yameitwa dhambi.

Mwili wako ni kama Farasi ambaye umempanda, mjali, mpende na mpe mahitaji yote.
Usimtese na wala usiweke uadui kushindana nae, Hutamshinda kwa namna karibu zote unazofikiri wewe. Na ukimshinda ujue kafa.
Mkubali asilimia zote kwa upendo ila USISHIKAMANE NAE, ukiweza utaitwa Nabii, mtakatifu n.k
Kushikamana ndo mzizi wa mateso karibu yote katika jamii ya binadamu, sio kushikamana na mwili tu bali na chochote kile.

#Kutoshikamana
#AmkaUangaze
#SelfRealization
#Spirituality
 
 

Share on Google Plus

About Unknown

NyangeTech inahamasisha maelfu na maelfu ya watu kujitambua kuelekea safari ya kuangaziwa ili kupata utulivu wa nafsi kwa kupata muunganiko na Mungu.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment