ANZA KUUTAFUTA UTU WAKO WA NDANI WA KIROHO KWANI UNA MAJIBU YOTE

Binadamu kaupigisha usingizi utu wake wa ndani, utu wake wa kale, Umezimika kabaki kama nyumba isiyo na taa. Giza totoro moyoni mwake hamna nuru tena. Hii ndio siri ya maisha kuonekana yanaboa, hii ndio siri ya maisha kua hayana maana. Muumbaji alikusudia binadamu afurahie maisha lakini kwa kulala usingizi mzito binadamu anayakosa maisha yaliyokusudiwa. Maisha ya furaha yapo muda wote hata sasa unavyosoma hapa yapo! lakini binadamu hawezi kuyapata akiwa usingizini ni lazima aamke. Ni lazima afumbue macho.

Kutokana na usingizi aliolala binadadamu na kuendelea kushikilia ndoto zake mbaya anaukosa uhalisia wa maisha na maisha pia anayakosa. Siku hizi watu wanaoishi wamekosekana, wamekua hadimu. wale wanaodhani wanaishi ukweli ni kwamba hawaishi bali wanasubiri kufa. 

Ndio!!! siku hizi kuishi hakupo ila kusubiri kufa kupo. Na ili  binadamu huyu asiye hai asiboreke sana anavyosubiri kufa anaona ajidanganye kushikamana na mwili wake, busy kutafuta umaarufu, pesa, mavazi, mahusiano, mvuto  na takataka chungu nzima ambazo si mbaya kuwa nazo lakini ndo hazimuhusu, zenyewe  ni za ziada tu lakini binadamu ndo anapotelea katika hizo na kushikamana nazo na anasahau yeye ni nani na kwanini yupo hapa, Binadamu huyu huona ajabu na kushtuka sana pale anapopata hayo yote halafu nafsi haitulii wala kuridhika.
Ndugu msomaji anza sasa kuutafuta utu wako wa ndani ukiupata utajazwa na kutoshelezwa, Mungu yupo humo na utulivu wa nafsi pia. 

#SelfRealization
#Kuangaziwa
#JourneyWithing
Share on Google Plus

About Unknown

NyangeTech inahamasisha maelfu na maelfu ya watu kujitambua kuelekea safari ya kuangaziwa ili kupata utulivu wa nafsi kwa kupata muunganiko na Mungu.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment